Mr Blue apinga kupigwa kwa wanawake kwenye ndoa

0
28

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mr Blue amefunguka na kusema kuwa yeye si mwanaume wa kumpiga ngumi mkewe bali anapiga kwa maneno.

Mr Blue amesema kuwa yeye hajawahi kumpiga mkewe hata kofi, bali anatumia maneno kumrekebisha.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa “Si jambo zuri kumpiga mwanamke, na katika maisha yangu, sijawahi kumpiga mwanamke, ila maneno yangu yanatosha kumchapa,’.

Kauli ya mwanamuzi huyo imekuja baada ya Shilole kuibua tuhuma za kupigwa na mume wake Uchebe, ambapo mastaa kadhaa wamekuwa wakijitokeza na kupinga tabia hiyo.

Mr Blue ana mke na watoto wawili hivyo amedai hawezi kumpiga mke wake kwani ni vitendo vya ukatili kuwapiga wanawake.

LEAVE A REPLY