Mpoto awavaa wanasiasa kuhusu wasanii

0
225

Mwanamuziki wa nyimbo za asili, Mrisho Mpoto amewaomba wanasiasa wawape nafasi ili wasanii nao waweze kupata muda wa kutambulisha kazi zao za sanaa kwa jamii ambayo sasa imetekwa na upepo wa siasa.

Hayo yameibuka kutokana na matukio makubwa ya kisiasa kila kukicha na baadhi ya wasanii wakiongozwa na Mpoto kuandika katika mitandao ya kijamii kuwataka wanasiasa wajaribu kidogo kupunguza kasi yao ili nao waweze kusikika.

 

Pia Mpoto amesema siyo kweli kwamba wanasiasa hawaelewi chochote wanachowafanya wasanii na watu wengine wanaotegemea upepo wa ‘promo’ katika kufanya na kutangaza kazi zao.

 

Msanii huyo amesema kwa sababu wanamsikia anawaomba kidogo ‘slow down’ ili vijana wao waweze ku-boost kazi zao kwa sababu ‘investment’ kubwa wameweka katika hizo shughuli, muda pamoja na fedha.

LEAVE A REPLY