Mpenzi wa Ben Pol afunguka mahusiano yao

0
148

Mpenzi mpya wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ben Pol aitwae Anerlisa amefunguka alipokutana na Ben Pol kwa mara ya kwanza mpaka kuanzisha uhusiano.

Mwanadada huyo ameweka wazi kuwa hajakutana na Ben Pol leo wala jana bali ni siku nyingi lakini wamekuwa marafiki kwa muda kabla ya kuwa wapenzi.

Wawili hao ambao wamekuwa wakisemwa sana katika mitandao ya kijamii hasa kutokana na status ya mwanadada huyo, anasema kuwa wamekutana muda mrefu kabla ya kuamua kuwa wapenzi.

Mwanadada huyo amesema kuwa walikutana mwezi wa tatu mwaka jana wakati Ben Pol alipokwenda Kenya kwa ajili ya kufanya ziara katika vyombo vya habari nchini humo.

Ben Pol na Anaerlisa kwasasa wapo katika mapenzi moto moto ambapo muda wote uonekana pamoja sehhemu mbalimbali wanapokuwa.

LEAVE A REPLY