Mpelelezi adai Wema alimuambia anavuta bangi kama starehe

0
157

Kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu imeendelea tena leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Mpelelezi katika kesi hiyo WP Marry amedai mahakamani kwamba msanii huyo alimwambia hajihusishi na kuuza dawa za kulevya ila anatumia bangi kwa starehe.

Mary ambaye shahidi katika kesi hiyo, amedai hivyo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipokuwa akitoa ushahidi akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Amedai Wema Februari 4, mwaka jana wakiwa ndani ya gari la polisi wakitokea Kituo Kikuu cha Polisi kuelekea nyumbani kwake Bunju Basihaya kwa ajili ya upekuzi ndipo alipomweleza hayo baada ya kumuuliza kama anahusika na kutumia dawa za kulevya ama kuuza.

Amedai kwa kuwa alikuwa anaongea na Wema hadhani kama askari wengine waliokuwapo kwenye gari walisikia, ila baada ya kuona Wema amekiri alimweleza OC CID Dennis Mujumba wakiwa ndani ya gari.

Wema anatuhumiwa kwa kosa la matumizi ya dawa za kulevya ikiwamo bango. Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Machi 12 na 13, mwaka huu kwa ushahidi wa upande wa jamhuri kuendelea na mashahidi wake.

 

LEAVE A REPLY