Moyes bosi mpya Sunderland

0
118
Manchester United's Scottish manager David Moyes looks on ahead of the UEFA Champions League Group A football match between Manchester United and Real Sociedad at Old Trafford in Manchester, northwest England on October 23, 2013. AFP PHOTO/ANDREW YATES (Photo credit should read ANDREW YATES/AFP/Getty Images)

Klabu ya soka ya Sunderland ya Uingereza imemtangaza rasmi mocha wa zamani wa Manchester United na Everton, David Moyes kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

David Moyes anachukua mikoba iliyoachwa na Sam Allardyce a.k.a Big Sam aliyeikacha timu hiyo baada ya kuisaidia kutoshuka daraja msimu uliopita na kuchukua jukumu la kuinoa timu ya taifa ya Uingereza maarufu kama Three Lions.

David Moyes amekubali kutia saini mkataba wa miaka minne wa kuinoa timu hiyo maarufu kama The Black Cat.

Klabu ya Sunderland ilitarajiwa kufanya uamuzi wa haraka wa kutafuta kocha mpya baada ya Allardyce kuonyesha dhahiri hamu ya kuinoa timu ya taifa na hivyo alipothibitishwa na FA kukabidhiwa mikoba hiyo hakusubiri hata kuaga.

Katika kuonyesha kutopendezewa na kitendo cha FA kumteua Big Sam kuinoa timu ya Uingereza, Sunderland kwenye taarifa yao ya kuthibitisha kuondoka kwa Allardyce hawakuonyesha shukrani yoyote kwa mocha huyo licha ya kuisaidia kwa kiasi kikubwa timu hiyo kutoshuka daraja msimu uliopita.

Moyes emerge kwenye ligi kuu ya Uingereza akita na kumbukumbu za kufukuzwa kazi akita na Manchester United, miezi kumi tu baada ya uteuzi wake.

LEAVE A REPLY