Mourinho: Martial anisikilize mimi na sio wakala wake

0
152

Kocha wa Man United, Jose Mourinho amemtaka mshambuliaji wa klabu hiyo, Anthony Martial amsikilize yeye na aache kusikiliza maneno ya wakala wake.

Wakala wa mshambuliaji huyo kwenye siku za karibuni alitoa maneno kuwa anamfanyia mpango mchezaji huyo kwenda kwa mkopo kwenye klabu ya Sevilla ya Hispania.

Martial mwenye miaka 21 ambaye siku ya jana alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi wakati United ilipotoka nyuma na kuifunga Middlesbrough 2-1 kwenye uwanja wa Old Trafford.

Martial alijiunga na Red Devils akitokea Monaco kwa ada ya £36m mwaka 2015 na kuwa mchezaji mdogo ghali zaidi.

‘Martial anapaswa kunisikiliza mimi na sio wakala wake. Anapaswa kunisikiliza mimi mazoezini na kufanyia kazi mrejesho ninaompa na kujibidiisha mazoeizini ili kukuza kipaji chake’.

LEAVE A REPLY