Mourinho ‘maji ya shingo’ Mkongwe Schweinsteiger arudishwa ‘kikosi cha kwanza’

0
197

Hatimaye mkongwe wa soka la Ujerumani na kiungo wa Manchester United, Bastian Schweinsteiger ameanza kufanya mazoezi na timu ya wakubwa kwa mara ya kwanza tangu kutua kwa Jose Mourinho.

Schweinsteiger, ambaye ameichezea United mechi 31 tangu kujiunga na miamba hiyo kwa thamani ya £14.4m akitokea Bayern Munich.

Jose Mourinho alimtahadharisha Schweinsteiger kuwa nafasi yake ndani ya kikosi cha Man United ni finyu na akamshauri atafute timu nyingine.

Hata hivyo baada ya kufungiwa kwa Ander Herrera baada ya kupewa kadi nyekundu kwenye mchezo na Burnely, Mourinho ameamua kumpa nafasi kiungo huyo mkongwe.

LEAVE A REPLY