Mourinho azidi kumvuruga Conte

0
115

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ametupa jiwe gizani tena, kuhusu makocha mbalimbali ambao wanalia kuwa na majeruhi kwenye timu zao.

Mourinho amesisitiza kuwa na mejeruhi sio sababu ya kupata matokeo mabaya na hii moja kwa moja inaonekana ni ujumbe wa meneja wa Chelsea Antonio Conte.

Mourinho amesema kama ingekuwa kulalamikia majeruhi ndio kigezo cha kupoteza mechi basi yeye alipaswa kulalamika kila siku kutokana na idadi ya majeruhi kwenye kikosi chake ambao pia ni wachezaji muhimu kwenye timu akiwemo kiungo Paul Pogba.

Kocha huyo raia wa Ureno alimshutumu kocha mwenzake Antonio Conte raia wa Italia kuwa analia sana kuhusu majeruhi wakati kila timu ina wachezaji wa akiba ambao wanaweza kutumika wakati ambao wengine wakiwa majeruhi.

Mvutano kati ya makocha hao wawili umeendelea kuimarika hususani wiki hii ambapo timu zao zitakutana jumapili ya kesho kwenye uwanja wa Stamford Bridge ukiwa ni mchezo wa 11 wa EPL msimu huu.

LEAVE A REPLY