Mourinho alichowaambia mashabiki wa Chelsea baada ya kumzomea

0
393

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amewaambia mashabiki wa Chelsea kwamba yeye bado ni “Number One” kwenye klabu hiyo baada ya kuzomewa wakati wa mechi iliyomalizika 1-0 katika uwanjani wa Stamford Bridge jana.

Mourinho, ambaye alikuzwa kazi mara mbili na Chelsea, aliitwa ‘Yuda’ na mashabiki wakati wa mechi hiyo.

Hata hivyo, aliwajibu kwa kuwaelekezea vidole vitatu, ishara ya mataji matatu ya ligi aliyoyashinda akiwa na klabu hiyo.

Alisema baadaye: “Hadi wampate meneja ambaye atawashindia mataji manne ya Ligi ya Premia, mimi bado ni nambari moja”.

Kwenye mechi hiyo Manchester walimaliza mechi wakiwa wachezaji 10 baada ya Ander Herrera kuonyeshwa kadi nyekundu dakikaya 35.

Mourinho, 54, ndiyo kocha aliyefanikiwa zaidi Chelsea baada ya kushinda mataji matatu vipindi viwili alivyokuwa Stamford Bridge mwaka 2005, 2006 na 2015.

 

LEAVE A REPLY