Morocco kujiunga tena AU

0
261

Umoja wa Afrika (AU) umesema Morocco imewasilisha rasmi ombi la kutaka kujiunga tena na muungano huo.

Morocco ilijitoa katika lililokuwa Shirika la Muungano wa Afrika OAU, zaidi ya miongo mitatu iliyopita kufuatia mzozo kuhusu eneo la Magharibi mwa Sahara

Muungano wa Afrika umelitambua eneo hilo kama taifa huru, wakati Morocco inalitazama kama sehemu ya eneo lake.

Inatarajia kuwa kwa kujiunga kwa mara nyengine na muungano wa Afrika itasaidia kuipa nafasi zaidi ya kushawishi mataifa mengine kuunga mkono msimamo wake kuhusu sehemu ya Magharibi mwa sahara.

LEAVE A REPLY