Moni Centrozone ampiga marufuku Nai kutumia nyimbo zake

0
13

Mwanamuziki wa hip hop Bongo, Moni Centrozone amempiga marufuku aliyekuwa mpenzi wake Nai kuacha kutumia nyimbo zake kwenye matamasha ya muziki.

Moni ameandika “NIMEKUWA NIKITUMIWA HIZI VIDEO NA KUPIGIWA SIMU KUTOKANA NA TABIA YA HUYU BINTI KUTUMIA NYIMBO ZANGU KUBURUDISHA KWENYE MATAMASHA MBALIMBALI. KISHERIA HAKI ZA KUUZA AU KUBURUDISHA KUPITIA KAZI ZA SANAA ANAYO MSANII HUSIKA ALIEZALISHA HIYO KAZI.

BINAFSI HUYU BINTI AMEKUWA AKINIKASHIFU KUNIPIGA VITA NA KUNIDHALILISHA KWENYE JAMII ILIONIZUNGUKA HADI WATU WA KARIBU LAKINI NIMESTAAJABU KUONA AKITUMIA KAZI ZANGU KWENYE MATAMASHA YA MUZIKI.

Pia ameendelea kuandika NAOMBA KUTOA ONYO KALI KWA UONGOZI WA AKIDA OG PAMOJA MENEJIMENTI NZIMA KUWA NI MARUFUKU BINTI YENU KUTUMIA KAZI ZA MAJENGO SOKONI (Moni Centrozone) NAOMBA HII TABIA IKOME MARA MOJA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NIMEONA NIWE MUUNGWANA KUTOA ONYO MAANA KWENYE SHERIA ITAWAGHARIMU NA MIMI SINA ROHO HIYO YA KUKOMOANA UKIZINGATIA NAIJUA HALI YAKE KIMAISHA HANA UWEZO WA KINILIPA INTELLECTUAL PROPERTY RIGHT.

NIMECHUKUA UAMUZI HUU KUTOKANA NA MASHABIKI ZANGU NA CABINET YA MAJENGO SOKONI KUTOFURAHISHWA NA KITENDO HIKO NAWAPENDA MASHABIKI ZANGU NA NAWAHESHIMU SANA.

LEAVE A REPLY