Moni Centrozone akanusha kumchana Nai kwenye ngoma yake mpya

0
24

Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Moni Centrozone amekanusha kumchana aliyekuwa mpenzi wake kwenye wimbo wake mpya uitwao ‘Maelezo Chapter 1’ uliotoka hivi karibuni.

Kutokana na maneno yaliyoimwa kwenye wimbo huo baadhi ya mashabiki wa wanasema kuwa mwanamuziki huyo kutoka pande za Dodoma amemchana aliyekuwa mpenzi wake Nai ambao kwa sasa wameachana.

Moni alikanusha hilo kwa kusema kwenye ngoma hiyo amejizungumzia yeye mwenyewe na sio mtu mwingine hivyo hakuna mtu ambaye ameimbwa kwenye ngoma hiyo.

Amesema kuwa “Nimejiongelea Mimi, naweza kusema kwa namna moja ama nyingine nimeji-diss mimi mwenyewe hivyo inatakiwa mtu asijistukie.

Pia amesema kuwa Nimeeleza yale mawazo ya watu ambayo wanayo kuhusu mimi, life style yangu, nilipotoka na ninavyo struggle na muziki wangu. Nimeelezea vitu vilivyonitokea na namna watu wana express vipi na kuonesha mimi nipo comfortable kiasi gani kuendelea na kazi.”.

LEAVE A REPLY