Monalisa na mwanawe wambwaga chozi

0
103

Muigizaji wa Bongo Movie, Yvonne Cherry maarufu kama Monalisa na Mtoto wake Sonia walishangaza watu Baada ya kuonekana wakiangua kilio mbele ya hadhara.

Monalisa na Mwanaye walishikwa na huzuni na kuanza kulia walipokuwa wakikabidhi misaada kwenye kituo cha kulea watoto yatima cha Yoko kilichopo Mbezi- Mwisho jijini Dar.

Aliyeanza kulia ni mtoto wa staa huyo, Sonia baada ya kupewa kipaza sauti azungumze ambapo alishindwa, akaanza kulia huku mama yake akimkumbatia, wakajikuta wakilia pamoja na baadae watoto wa kituo kile nao walionekana wakilia.

Rafiki wa karibu wa Sonia ambaye alikuwa ameongozana nao alitoa sababu iliyomfanya mpaka akaanza kulia katika kituo hiko.

Monalisa alifunguka na kusema kuwa ameamua kujitoa kusaidia wazo hilo la mtoto wake kwa sababu ameona anafanya jambo jema.

LEAVE A REPLY