Monalisa ashinda tuzo nchini Ghana

0
126

Muigizaji wa Bongo Movie, Monalisa ameshinda tuzo ya The African Prestigious Awards (APA) 2017 kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Kike barani Afrika.

Tuzo hizo zilizotolewa usiku wa kuamkia leo mjini Accra nchini Ghana ambapo muigizaji huyo ameibuka mshindi.

Waigizaji wengine kutoka Tanzania aliyoshinda tuzo hiyo ni Ray ambapo ameshinda tuzo ya muigizaji bora wa kiume barani Afrika.

Mtanzania Moise Hussein ameshinda tuzo hizo kwenye kipengele cha mpiga picha bora barani Afrika kwa mwaka 2017.

LEAVE A REPLY