Monalisa afungukia umaarufu wa mtoto wake

0
35

Muigizaji mkongwe wa Bongo Movie, Yvonne Cherry maarufu kama Monalisa amefunguka kuwa, mwanaye Sonia alikuwa staa tangu anazaliwa.

Monalisa au Mona amesema umaarufu wa Sonia unaweza ukawa hujaanza kipindi hiki alichoanza kuimba Bongo Fleva, bali ni wa tangu anazaliwa.

Monalisa amesema kuwa “Unajua Sonia amekuwa maarufu tangu anazaliwa, yaani alikuwa anatoka sana kwenye magazeti, kipindi hicho ndoa yangu na marehemu George Tyson ambaye ni baba yake.

Monalisa ambaye mama yake mzazi ni Natasha amesema kuwa kwenye familia yao imejaliwa vipaji vingi kuanzia mama yake, yeye mwenye mpaka mtoto wake.

Mtoto wa Monalisa Sonia kwasasa amejipatia umaarufu kutokana na kipaji chake cha uimbaji kinachowavutia watu wengi sana hapa nchini.

LEAVE A REPLY