Monalisa afunguka siri ya urembo wake

0
186

Muigizaji wa Bongo Movie, Monalisa amesema kuwa hawezi kuzeeka kwa sababu hana kabisa stress na ndiyo maana kila siku anaonekana mrembo.

Kauli ya muigizaji huyo imekuja baada ya kuulizwa swali kuwa kwanini anaendelea kuwa mrembo japokuwa umri wake umeenda.

Monalisa amesema kuwa mara nyingi amekuwa akiulizwa swali la nini anatumia kiasi cha kumfanya asizeeke lakini anaeleza kwamba siri ya kuwa hivyo ni kutokana na muda mwingi kuwa na furaha na kutokuwa na stress za maisha.

Amesema kuwa “Mimi kwa kweli sina stress na sio kwamba sina matatizo ila niliamua sio kila jambo baya au linaloniumiza nalibebe, huwa naamua kuyapotezea kwa sababu nikisema nibebe dunia hii kuna mambo mengi, nitazeeka bure.

Pia amesema kuwa mara, nyingi amekuwa na mbinu nyingi za kutafuta nini cha kufanya ili kichwa chake kiwaze kazi na sio kushindwa au kuwaza kitu ambacho kitamfanya akose amani.

LEAVE A REPLY