Monalisa afunguka mwanawe kusoma nje nchi

0
44

Muigizaji wa Bongo Movie, Yvonne Cherry almaarufu Monalisa au Mona anasema kuwa, anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa mwanawe, Sonia George kwenda masomoni nchini Ukraine.

 

Monalisa amesema kuwa amefurahi mwanawe kusoma nje ya nchi kwa sababu maombi yake ya kila siku yalikuwa ni hayo hivyo Mungu amejibu, kwa hiyo acha tu aende maana ya walimwengu yalikuwa ni mengi.

 

Mona anasema kuwa, Sonia alipitia changamoto nyingi kipindi cha mwisho, lakini Mungu ni mwema amemjaalia kumaliza kidato cha sita na kupata nafasi za juu katika masomo yake.

 

“Amepitia changamoto nyingi, watu hawajui tu, ninamuombea kwa Mungu, aende tu, Mungu amjalie asome kwa bidii, akae mpaka amalize chuo, mimi mama yake niendelee kupigana na maisha, maana mambo ya walimwengu yalikuwa ni mengi sana,” anasema Mona.

LEAVE A REPLY