Monalisa achukizwa kuitwa ‘bibi’

0
107

Muigizaji wa Bongo Movie, Monalisa amewachamba wanaomuita ‘Kibibi’ baada ya kutokea kwenye video ya msanii wa Bongofleva Ben Pol, ambayo inakwenda kwa jina la Ntala Nawe.

Mona amesema kuwa hakushtushwa na ‘comment’ za mashabiki  wa Ben Pol ambao baada ya kuona video hiyo walianza kuhoji  kuwa kwa nini Ben Pol hajachukua wasichana wadogo na kumuweka yeye.

“Kila mtu ana mtazamo wake na kwangu mimi hicho ni kitu cha kawaida  watu lazima tu wataongea midomo wameumbiwa ili kuongea ila poleni sana na itabidi tu muiangalie video kwa sababu Ben Pol ndio mtu ambaye amenichagua na ameona ninapendeza kwenye video yake” alisema.

Monalisa aliongeza kuwa alikuwa tayari kufanya video hiyo bure bila malipo yoyote kwa kuwa anamkubali Ben Pol lakini msanii huyo alimpa kiasi fulani cha pesa na alimwambia thamani aliyonayo ni kubwa sana na anajua hatoweza kumlipa kiasi kinachoweza kufikia thamani hiyo.

Alimaliza kwa kusititiza kuwa ‘hawezi kukataza mitazamo ya watu kwani si kila mtu atapenda utakachokifanya”.

LEAVE A REPLY