Mogadishu: Watu watano wauawa kwa bomu Somalia

0
206

Watu watano wameuawa baada ya omu kulipuka nje ya hoteli moja katikati ya mji wa Mogadishu nchini Somali karibu na lango la jumba la rais nchini humo.

Kundi la wapiganaji wa Alshabab limekiri kutekeleza shambulio hilo katika mji huo.

Mtu mmoja aliyeshuhudia mlipuko huo amesema kuwa ameona watu wengi wakiwa wamejeruhiwa.
Huku akisema kuwa hoteli hiyo imeharibika vibaya na kwamba vikosi vya usalama vimewasili katika eneo hilo.

Vyombo vya habari vinasema kuwa mkutano wa usalama ulitarajiwa kufanyika katika hoteli hiyo ya SYL.
Hoteli hiyo imeshambuliwa mara kadhaa na al-Shabab katika miaka ya hivi karibuni na kusababisha uaribufu mkubwa.

LEAVE A REPLY