Mobetto ndani ya penzi jipya

0
102

Baada ya mwanamitindo Hamisa Mobetto kumuweka hadharani mpenzi wake Mmarekani kupitia akaunti yake ya Instagram sasa penzi kati yao linaonekana kushamiri na hii ni kutokana na video ambazo, mwanadada huyo amechapisha kwenye ukurasa wake.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Hamisa amepost video akiwa na Mpenzi wake na kuandika kuwa bila mpenzi wake huyo hawezi huku akijinadi kuwa penzi lake lina raha sana.

“Ila Penzi Letu Raha Sana, ila mimi bila huyu siwezi jamani, yaani hapo nimepakatwa na anavyo nitazama Yaraab”.

Hamisa Mobetto mpaka sasa bado yupo nchini Marekani na haijajulikana ni kwa muda gani wamefahamiana na mpenzi wake huyo na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi, huku ikielezwa kuwa penzi wake huyo ambae jina lake halisi Josh Adeyeye ni mcheza kikapu nchini Marekani.

LEAVE A REPLY