Mobetto adai ajazaa na Diamond kisa pesa

0
109

Mwanamitindo na Msanii wa Bongo fleva Hamisa Mobetto amefunguka na kuweka wazi kuwa hajazaa na Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz na mkurugenzi wa EFM kisa pesa kwani ana pesa zake binafsi.

Hamisa amesema watu wengi wakisikia amezaa na wanaume wenye uwezo kama hao basi moja kwa moja wanafikiri kuwa amefuata pesa Lakini hawajui kuwa pesa zake anatafuta mwenyewe kwa jasho lake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Hamisa amekana stori za kuwa amegeuza watoto wake mtaji kwa kuishi kutegemea matunzo atakayopewa kwa ajili ya Watoto Wake na Diamond pamoja na Majizzo.

Pia amesema kuwa yeye ni mtu ambaye alikuwa anajiweza vizuri tu kabla ya kuzaa na aninataka wasichana wadogo wanaomuangalia wajue kuwa kuzaa ndio kutoka kimaisha hapana sio hivyo.

Hamisa ameshawahi kusemekana kupangishiwa jumba la kifahari na baba wa Mtoto Wake Diamond Platnumz na kabla ya kuhamia hapo anadaiwa kuwa alipangishiwa nyumba na Majizzo.

LEAVE A REPLY