Mobeto: Sina mahusiano na Diamond Platnumz

0
529

Mwanamitindo maarufu nchini, Hamisa Mobeto amefunguka kwa kusema kwamba hana mahusiano ya kimapenzi na staa wa Bongo fleva, Diamond Platnumz zaidi ya kufahamiana kikazi tu.

Mwanamitindo huyo amesema tetesi zilizokuwa zinasambaa katika mitandao ya kijamii ni uzushi mtupu kwani hana mahusiano wala ukaribu na staa huyo kutoka kampuni ya WCB.

Hamisa Mobeto ameongeza kwa kusema kwamba kwa mara ya kwanza kukutana na Diamond ilikuwa katika Hotel ya Serena wakati akizindua nyimbo yake ya Number One.

Mara nyingi mwanamitindo huyo uonekana katika matukio kadhaa ya Diamond Platnum ambapo mashabiki wake wanajiuliza nani anampa mualiko ni Diamond mwenyewe au ndugu zake.

LEAVE A REPLY