Mobeto afunguka yaliyojiri Mahakamani jana

0
316

Mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto amefunguka sakata la malezi ya mtoto wake kutoka kwa baba yake Diamond Platnumz baada ya jana kufika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Hamisa Mobeto amesema kuwa ameamua kufungua shauli hilo mahakamani hapo ili apate haki ya mtoto wake kutoka kwa baba yake ambaye ni Diamond Platnumz.

Diamond Platnumz na Hamisa Mobeto jana walifika katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam upande wa watoto kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.

Pia Hamisa amesema kuwa hawezi kuongelea yote yaliyojiri kwenye kesi hiyo ila anamshukuru mungu wameelewana na baba mtoto wake kuhusu malezi ya mtoto wao baada ya kukutana mahakamani hapo.

Mwanadada huyo amesema kuwa kwa upande wake hana ugomvi na Diamond ili alikuwa anataka kuweka mambo sawa ndiyo mana aliamua kupeleka suala hilo mahakamani.

LEAVE A REPLY