Mo J ashangazwa na Gigy Money baada ya kuambiwa mtoto si wake

0
423

Aliyekuwa mpenzi wa video vixen Bongo, Gigy Money, Mo J amefunguka na kusema kuwa ameshangazwa na kitendo cha Gigy Money kusema mtoto aliyezaa nae si wa kwake.

Mo J amesema kuwa yupo tayari kupima DNA ili kuthibitisha kama mtoto huyo ni wake kweli au si wake kama Gigy Money alivyosema.

Amesema kuwa mtoto huyo ni wa kwake kabisa kwasababu yeye ndiyo alikuwa mtu wake na hakuwa na mtu mwingine.

Kwasasa Gigy Money anaishi na mwanaume mwingine ambae ana pesa kuliko Mo J na kwa madai ya Gigy Money ni kwamba Mo alikuwa akilea mimba siku nyingi akijua kuwa sio ya kwake.

Wawili hao kwasasa wametengana na kila mmoja anaishi maisha yake baada ya kugombana siku chache zilizopita.

LEAVE A REPLY