Mnara wa kuwakumbuka wanafunzi wa Lucky Vicent wajengwa jijini Arusha

0
106

Baada ya mwaka mmoja toka kutokea kwa ajali iliyoua wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent jinini Arusha, umejengwa mnara wa kuwakumbuka wanafunzi hao, walimu wao na dereva.

Ajali hiyo ilitokea Mei 6, 2017 ambayo iliua wanafunzi 29, dereva na walimu wawili huko katika mlima Rhotia wilayani Karatu Mkoani Arusha.

Jana May 6 ilikuwa ni kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kutokea kwa ajali hiyo iliyobakiza wanafunzi watatu tu waliokuwa kwenye basi hilo.

Katika kumbukumbu hiyo shule ya Lucky Vincent imefanya ibada maalumu ya kuwakumbuka wanafunzi pamoja na waalimu waliofariki kwenye ajali hiyo.

Umejengwa mnara katika eneo la mlima huo wa Rhotia ambapo ndipo gari hilo lilipopata ajali. Mnara huo una majina ya watoto wote waliofariki kwenye ajali hiyo.

LEAVE A REPLY