Mkurugenzi wa Kinondoni hawajia juu viongozi wa vyama

0
98

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli amewalaumu viongozi wa vyama kushindwa kutekeleza wajibu wao baada ya baadhi ya mawakala wao kuondolewa vituoni.

Mkurugenzi Aron Kagurumjuli ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi Kinondoni amesema kwamba baadhi ya vyama wameshindwa kuwapa barua za utambulishomawakala wao na kutaka kutumia barua za kiapo kama utambulisho.

Mkurugenzi huyo amesema wao kama wasimamizi jukumu lao lilikuwa kutoa barua hizo na pia ni jukumu la viongozi wa vyama kuhakikisha kuwa wanatekeleza wajibu wao kwani huwa ni rahisi kwa wao kukutana na mawakala wao kwani mpaka mawasiliano yao wanakuwa wanayo.

Aidha Mkurugenzi huyo ameweka wazi sababu za wao kutoa barua za utambulisho saa tano usiku ni kuhofia barua hizo kugushiwa.

Hata hivyo amethibitisha kuwa dosari hizo zimeshamalizika na hali ya vituo ni shwari hivyo wananchi wasisite kwenda kupiga kura.

Jimbo la Kinondoni, Siha na kata nane nchini leo yameingia katika zoezi la kupiga kura za kuchagua wabunge watakaoweza kuwakilisha shida za wananchi wa majimbo hayo Bungeni.

LEAVE A REPLY