Mkurugenzi wa halmashauri ya Kongwa afariki dunia wa ajali ya gari

0
463

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kongwa mkoani Dodoma, Mhandisi Ngusa Izengo anadaiwa kufariki dunia baada ya gari lake kuangukiwa na lori la mafuta usiku wa kuamkia leo katika eneo la Chalinze Nyama nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Giles Muroto alipokuwa anazungumza na mwandishi wa habari hii na kusema atatoa taarifa kamili baada ya kukamilisha.

 Kama Muroto amesema kuwa atatoa taarifa Zaidi hapo baadae “Nitatoa taarifa kamili zoezi hili uokaji litakapomalizika maana mpaka muda huu tumetoka eneo la tukio tumeshindwa kujua kuna watu wangapi ndani ya gari hilo lililoangukiwa.

Pia amesema kuwa “Tunaenda TAMESA kutafuta ‘grinder machine’ ilituweze kujua idadi kamili ya miili iliyopo ndani ya gari”.

 

LEAVE A REPLY