Mkojo wa Masogange wagundulika kuwa na chembechembe za madawa ya kulevya

0
293

Kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Video queen, Agnes Gerald ‘Masogange’ imeendelea leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo mahakama imeelezwa kuwa mtuhumiwa huyo alifanyiwa vipimo vya kemikali kupitipia mkojo wake kwa kutumia kifaa maalum na kugundulika kuwa na chembechembe  za madawa ya kulevya aina ya heroine.

Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.

Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14,2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).

Kesi hiyo imehairishwa hadi Agosti 28 mwaka huu itakapotajwa tena kwa ajili ya kusikiliza hukumu.

LEAVE A REPLY