Mke wa mtu amponza Tunda Man

0
586

Mwanamuziki nyota wa Bongo fleva kutoka kundi la Tip Top Connection, Tunda Man amesema kwamba ameshindwa kuachia video ya wimbo wake mpya ‘Mwanaume Suruali’ baada ya kumtumia mke wa mtu kama video queen.

Tunda Man amesema kuwa ameshindwa kuachia kazi hiyo kutokana na mume wa mwanamke huyo kuzuia video hiyo isitoke.

Tunda Man amesema “Kuna video ya wimbo wangu mpya ‘Mwanaume Suruali’ ambayo ilikuwa itoke hivi karibuni lakini kwa bahati mbaya mume wa video queen ambaye ametumika kwenye video amezuia video isitoke,”.

Pia Tunda aliongeza kwa kusema “Kwa hiyo bado tupo kwenye mazungumzo, kama akiruhusu itoke video itatoka hivi karibuni,”.

Mwanamuziki huyo amesema video hiyo itafanywa tena upya ili kuzuia matatizo yasitikee baada ya kutumia mke wa mtu kwenye video ya wimbo huyo mpya.

LEAVE A REPLY