Mkali wa rap, Frida Aman awashangaa wanaume kutomuelewa

0
300

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Frida Aman amesema pamoja na kujituma kwa kucheza kama mwanamke kwenye nyimbo zake lakini bado wanaume wameshindwa kumuelewa.

Frida amesema kuwa wanaume wengi wanahisi si mwanamke mlaini ambaye wanaweza kumfikia na kuanzisha naye mahusiano.

Frida amesema familia yake wote wameokoka na yeye pia ni mwokovu japo watu wengi wanamuangalia kwa jicho lingine na kumuwekea mambo mengi katika maisha yake ya kila siku wakati kuna baadhi ya vitu ambavyo hawezi kufanya kabisha kutokana na imani ya dini yake.

“Siwezi kufanya aina ya muziki anaoufanya rapa mwenzangu Rosa Ree na naamini hata Rosa hawezi kufanya aina ya muziki ninaoufanya mimi kwa kuwa tunatofautiana katika sanaa zetu na kila mmoja wetu ana aina tofauti ya muziki anaoufanya”.

Frida amemalizia kwa kuwaomba mashabiki zake kuendelea kumsapoti katika kazi zake za muziki anazozitoa ambapo kwa sasa ana nyimbo yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Pullup’ ambayo amemshirikisha rapa chipukizi Gifted, ambayo inafanya vizuri hivi sasa nchini.

LEAVE A REPLY