Mkaguzi wa fedha za serikali afungwa mwaka mmoja Misri

0
116
Mkaguzi mkuu wa zamani wa hesabu za serikali amnaye alifutwa kazi baada ya kuituhumu serikali kwa rushwa amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kusambaza ‘habari za uongo’.
Mkaguzi huyo, Hisham Geneina alifukuzwa kazi mwezi Machi mwaka huu baada ya kukadiria hasara ya $67.6bn (£51.3bn) kutokana na rushwa ndani ya miaka minne.
Rais wa nchi hiyo, Abdul Fattah al-Sisi alimfuta kazi Hisham kisha akafunguliwa mashtaka ya kusambaza habari za uongo baada ya rais al-Sisi kuunda tume ya kutafuta ukweli ambayo ilidai makadirio yaliyofanywa na Hashim ni makubwa.
Hisham amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani na kulipa faini ya $2,200 au anaweza kulipa faini pekee ya jumla ya $3,300.
Wakili wa Hisham, Ali Taha amedhamiria kukata rufaa kwa madai kuwa waendesha mashtaka wameshindwa kuthibitisha madai yao na pia hoja za mlalamikiwa hazijachunguzwa.
Wakati hukumu yake ikitolewa kwenye mahakama ya Cairo, waandishi wa habari walizuiwa kuhudhuria.
Jaji wa zamani wa nchi hiyo, Geneina ameyakataa mashtaka aliyoshitakiwa nayo Hisham na kusema yamepatikana kisiasa.
Mashtaka aliyofunguliwa Hisma yametokana na kauli yake kwa magazeti mawili ya Misri, al-Youm al-Sabea ambalo lilimuhoji mwezi Disemba mwaka jana wakati akiwa mkuu wa ofisi ya mamlaka ya uwajibikaji wa taifa (ASA).

LEAVE A REPLY