Mjomba wake Mane ahofia usalama wake nchini Senegal

0
240

Mjomba wake NA mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane, Sana Toure amesema kuwa anahofia usalama wa familia yake baada ya Mane kukosa penati na kusababisha Senegal kutolewa kwenye mashindano ya Afcon yaliyomalizika nchini Gabon.

Sana Toure amesema kuwa gari ambalo alikuwa amenunuliwa na mpwa wake Mane, ambaye ndiye mchezaji ghali zaidi barani Afrika, liliharibiwa na nyumba yake kulengwa.

Mjomba wake amesema “Siku baada la Lions kuondolewa, baadhi ya watu walio na nia mbaya wakataka kuvamia nyumba yangu iliyo Malika. Nawashukuru majirani na wenyeji, kitu kibaya kilizuiwa,”

Sadio Mane anaonekana kusahau yaliyomsibu Afcom na kufunga mara mbili Liverpool ilipokutana na Tottenham wikendi hii.

LEAVE A REPLY