Miujiza kuipeleka Yanga nusu fainali (CAF)

0
122

Mabao mawili ya straika Mohammed Abass imeisaidia timu ya Medeama ya Ghana kupata ushindi wake wa kwanza kwenye kundi A la michuano ya kombe la Shirikisho la soka Afrika (CAF) kwa kuigalagaza Yanga ya Tanzania kwa jumla ya mabao 3-1.

Pambano hilo lililofanyika kweye uwanja wa Sekondi-Takoradi usiku wa jana limeisaidia Medeama kufikisha pointi 5 baada ya kucheza michezo minne sawa na MO Bejaia ambao wamecheza mechi tatu na wanatarajia kupambana na vinara wa kundi hilo, TP Mazembe jioni ya leo.

Yanga imesalia na pointi yake moja baada ya kucheza nne huku ikipoteza mechi tatu na kutoa suluhu moja.

Kundi A linaongozwa na TP Mazembe ikiwa na pointi saba kutokana na mechi tatu na watajihakikishia kupenya hatua ya makundi na kutinga nusu fainali endapo itawafunga Mo Bejaia baadae leo.

Medeama walainza kuandika mabao yao dakika ya saba ya mchezo kupitia kwa mchezaji Daniel Amoah. Dakika ya 22 Medeama waliongeza bao la pili kupitia kwa Mohammed Abass kabla ya Yanga kupata penati iliyotumiwa vizuri na Simon Msuva kabla ya Abass tena kuaindikia timu yake bao la tatu kwenye dakika ya 37.

Yanga wataikaribisha MO Bejaia Agosti 13 kabla ya kumalizia mechi zake na TP Mazembe jijini Lubumbashi nchini Congo.

Ili kufuzu kwa hatua ya makundi, timu ya Yanga atalazimika kuwafunga MO Bejaia Agosti 13 kisha kuwafunga TP Mazembe kwenye pambano la marudiano jijini Lubumbashi.

Wakati huo huo ikiomba TP Mazembe washinde mechi zake mbili kati ya MO Bejaia (leo jioni) kisha wawafunge Medeama na dua zao zinaomba pia pambano kati ya MO Bejaia na Medeama limalizike kwa sare.

LEAVE A REPLY