Miss Tanzania kuingia kwenye filamu

0
67

 

Miss Tanzania mwaka 2018, Queen Elizabeth Makune ametangaza rasmi kwamba yupo tayari kuingia kwenye filamu za Bongo Movie na muziki wa Bongo fleva.

Queen Elizabeth aliibuka kidedea kwenye mashindano ya Miss Tanzania miezi  michache iliyopita na kuenda kuiwakilisha Tanzania katika shindano la Miss world China.

Miss Tanzania huyo amejigamba kuwa atafanya chochote kwa kuwa ana uwezo katika kazi zote alizotaja alisema kuwa, hawezi kujifunga kwenye kitu kimoja na siku zote ana imani kwamba wanaofanikiwa wengi wanafanya vitu zaidi ya kimoja.

Kuhusu kushindwa kufika mbali  kwenye mashindano ya Miss World yaliyofanyika hivi karibuni Sanya nchini China, mrembo huyo hakuwa tayari kuongea lolote akidai haukuwa muda muafaka.

LEAVE A REPLY