Miss Tanzania afunguka baada ya kukosa taji la Miss World

0
233

Miss Tanzania, Queen Elizabeth Makune amefunguka kwa mara ya kwanza tangu arudi nchini kutokea nchini China kwenye mashindano ya Miss World.

Mashindano ya Miss World yalifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita huko Sanya nchini China ambapo mrembo kutoka Mexico Vanessa Ponce de Leon ndiye aliyetawazwa kuwa Miss World.

Japokuwa Miss Tanzania hakufanya vizuri sana na kutoka katika hatua za mwanzoni za mashindano lakini watu wengi walionekana juhudi zake katika kutaka kushinda.

Amesema kuwa anawashukuru watanzania kwa mchango wao, pia amejifunza mengi nchini China na anashukuru kwa matokeo aliyoyapata.

LEAVE A REPLY