Mishahara serikalini Tanzania kutolewa kwa vyeti?

0
646

Baadhi ya watumishi wa umma nchini Tanzania huenda wakakosa mishahara yao ya mwezi Julai kufuatia zoezi jipya la ukaguzi wa nakala halisi za vyeti vyao vya elimu na nyaraka za ajira.

Huo ni mkakati wa kudhibiti wimbi la wafanyakazi hewa kwenye serikali ya awamu ya tano ambapo mpaka sasa zaidi ya wafanyakazi hewa 3,000 wamegundulika.

Bado haijajulikana iwapo amri rasmi ya kufanya hivyo imeshatolewa lakini kwa mujibu wa shirikka la BBC tayari baadhi ya idara za serikali ikiwemo baadhi ya wizara zimeshawataarifu wafanyakazi wake.

Waziri wa TAMISEMI Angellah Kairuki amewahi kunukuliwa akisema kuwa maofisa 3,600 kwenye mkoa wa pwani hawatopata mishahara yao kutokana na kushindwa kutimiza sharti hilo.

Tayari vyama vya wafanyakazi vimeanza kupinga amri hiyo vikidai kuwa inakiuka haki ya mfanyakazi kupata mshahara.

Kama amri hiyo itathibitishwa na serikali, itakuwa ni muendelezo wa jitihada za serikali ya awamu ya tano kudhibiti upotevu mkubwa wa fedha za umma ambao rais Magufuli amenukuliwa mara kadhaa kusababishwa na wafanyakazi hewa.

LEAVE A REPLY