Mimi Mars atoa ya moyoni

0
47

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mimi Mars ameyatoa yake ya moyoni kwa wadau wa muziki nchini Tanzania ambao wanawasapoti wasanii wa nje Zaidi kuliko wa ndani.

 

Mimi Mars amesema hayo kwasababu baadhi ya mashabiki na wadau hawawaheshimu wasanii wa ndani ya nchi, badala yake wanawaheshimu na kuwashobokea wale wanaotoka nje ya Bongo.

 

Kupitia Insta Story yake, Mimi Mars ameandika; “Kwa yeyote itakayemhusu; inabidi muanze kuwapa heshima inayostahili wasanii wenu wa nyumbani zaidi hata ya wasanii mnaowaleta kutoka nchi za nje. Ifike mahali wasanii tupaze sauti…”

 

Hata hivyo, Mimi Mars hajaweka wazi zaidi ni kitu gani ambacho kimemsababisha aseme hivyo, lakini wadukuzi wamesema ujumbe umewafikia wahusika.

LEAVE A REPLY