Mimi Mars akanusha Vanessa Mdee kuwa na Mimba

0
20

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mimi Mars ametupilia mbali tetesi na uvumi ambao umekuwa ukienea kuwa dada yake, Vanessa Mdee kwa sasa ana mimba ya mchumba’ke, Rotimi.

Mimi Mars ameanika ukweli kwamba, Vanessa au Vee hana mimba kama watu wengi wanavyoeneza kwenye kurasa za udaku za Instagram kwa kumuangalia tu Vanessa kwenye picha.

Mimi Mars amesema kuwa Vanessa Mdee angekuwa na ujauzito angekuwa ameshamwambia kwani ni mtu ambaye anazungumza naye mambo mengi kuanzia kikazi, kifamilia na hata mambo yao ya siri wanashirikishana.

“Ukweli ninao mimi, Vee hana mimba, angekuwa nayo angeshaniambia,” anasema Mimi Mars ambaye ni mdogo wake na Vanessa Mdee.

Mimi anasema kuwa, wakati wa Vee kupata ujauzito ukifika atafanya hivyo. Hii ni mara ya pili kwa Vanessa kusemekana kuwa ni mjamzito.

LEAVE A REPLY