Mimi Mars akanusha kutoka kimapenzi na Marioo

0
358

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mimi Mars amekanusha kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Mwanamuziki mwenzake Marioo baada ya taarifa kusambaa mtandaoni.

Mimi Mars amekanusha taarifa hizo baada ya kusambaa katika mitandao ya kijamii kuwa wawili hao wanatoka kimapenzi jambo ambalo mwanamuziki huyo amelipinga vikali kwa kusema kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki huyo.

Mwanamuziki huyo ameendelea kusema kuwa hana mahusiano na Marioo isipokuwa ni rafiki yake kikazi lakini hakuna kitu kinachoendelea kati yao kuhusu mahusiano hivyo habari zinazosambazwa hazina ukweli wowote.

Pia Mimi Mars amesema kuwa sababu inayofanya watu wasambaze habari ni baada ya watu kutomjua mpenzi wake inapelekea hali hiyo ya baadhi kuhisi anayeonekana kuwa karibu naye ni Mpenzi wake jambo ambalo sio kweli.

Wawili hao ni miongoni mwa wasanii ambao wanaonekana wakiwa pamoja kwa muda mrefu mpaka kupelekea watu kuhisi kuwa wawili hao wana mahusiano ya kimapenzi kati yao.

LEAVE A REPLY