Mgao wa $1bn wa Mirabaha wa YouTube ‘hautoshi’?

0
166

Pale unaposikia hapa Tanzania media zinazolipa mirabaha ni tatu tu, lazima ushangae na ushike mdomo; kwanini? Kuna media zaidi ya 200 iweje zilipe 3 tu?

 Lakini ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni.

Wadau wa muziki nchini Marekani wamedai kuwa mgao uliotolewa na mtandao wa YouTube wa $1bn (TZS 2.1trn) ni ‘kiduchu’.

Mkurugenzi wa biashara wa YouTube, Robert Kyncl alipost kwenye blog kuwa mtandao wake umelipa kiasi hicho cha pesa kwenye tasnia ya muziki ambapo hata hivyo watu wengi hu-download video za muziki bure.

Hata hivyo lebo za muziki chini ya umoja wao wa IFPI, hazijakubaliana na hoja hizo na kudai maelezo ya mkurugenzi huyo yalikuwa hayajitoshelezi.

YouTube wamedai wamepata fedha kiasi cha $1 kwa kila mtumiaji anayelipia lakini IFPI wamedai sio kweli kwasababu mtandao mdogo wa Spotify mwaka 2015 ulilipa $2bn (TZS 2.2trn) ambazo ni sawa na $18 kwa kila mtumiaji anayelipia.

Hata hivyo YouTube wameahidi kuboresha mfumo wao wa sasa wa ukusanyaji fedha ili kukuza mirabaha yao.

LEAVE A REPLY