Mfahamu Cheick Tiote aliyefariki akiwa mazoezini

0
258

Kiungo wa zamani wa timu ya Newcastle United, Cheick Tiote amefariki dunia akiwa an miaka 30 baada ya kuzimia wakati wa mazoezi nchini China.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alikaa miaka saba Newcastle na kuwachezea mechi 138 za ligi.

Alihamia klabu ya Beijing Enterprises mwezi Februari mwaka huu akitokea Newcastle United ya nchini Uingereza.

Tiote alizaliwa Ivory Coast na alikuwa kwenye kikosi kilichoshinda Kombe la Mataifa ya Afrika 2015.

Alianza uchezaji wake wa soka ya kulipwa Ubelgiji akiwa na klabu ya Anderlecht mwaka 2005 kabla ya kuhamia FC Twente ya Uholanzi ambapo alicheza mechi 86 na kushinda taji la ligi ya Eredivisie msimu wa 2009-10 chini ya meneja Steve McLaren.

Tiote, ambaye ni kiungo wa kati mkabaji, kisha alihamia Newcastle mwaka 2010 kwa £3.5m na kuwa mchezaji tegemeo wa klabu hiyo.

Mwaka 2011, alifunga bao linalokumbukwa sana alipowasaidia Newcastle United kujikwamua kutoka 4-0 chini Ligi ya Premia dhidi ya Arsenal na kutoka sare.

LEAVE A REPLY