Merkel: ‘Tutapokea wahamiaji licha ya vitisho vya ugaidi’

0
83
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ametetea sera za nchi hiyo kuhusu wakimbizi na kusema hazitobadilishwa licha tishio la hivi karibuni la matukio ya ugaidi.
Kwenye taarifa yake, Bi. Merkel amewashangaa baadhi ya watu wanaoomba hifadhi nchini humo kuwa miongoni mwa watu wanaokosoa sera zake dhidi ya wakimbizi.
Merkel amesisitiza kuwa mtu yeyote anayekimbia mauaji na vita anayo haki ya kulindwa.
Bi. Merkel mependekeza hatua za kuimarisha usalama ikiwemo upashanaji wa taarifa, udhibiti wa uuzaji wa silaha kwa njia za mitandao  na kuongeza hatua za kiulinzi kwenye kukabiliana na mashambulizi.
Mashambulizi mawili ya hivi karibuni ya Bavaria yalifanywa na watu wanaoomba hifadhi.
Shambulizi la kujitoa mhanga la Jumapili ambalo lilijeruhi watu 15 lilifanywa na raia wa Syria ambaye amenyimwa hifadhi nchini humo lakini amepewa kibali cha muda cha kuishi.
Pia tukio la shambulio la kutumia shoka na kisu lililotokea kwenye treni kwenye mji wa Wuerzburg Julai 18 July pia limefanywa na muombaji wa hifadhi kutoka Afghanistan.
Bi. Merkel amesisitiza kuwa Ujerumani ‘itasimama kwenye misingi yake’ kwenye kuwapa malazi watu wanaostahiki.
‘Mashambulizi ya Ujerumani na yale ya Ufaransa yalilenga kusambaza hofu na chuki baina ya tamaduni na baina ya dini’ Amesema Merkel.
Akizungumza kwenye mji mkuu wan chi hiyo, Berlin, Bi. mMerkel amedai kuwa ‘mbali ya mashambulizi ya kigaidi yanayopangwa, kutakuwa na vitisho vingine kutoka kwa waovu ambao hawajulikani na watu wa usalama’.
‘Kukabiliana na haya tunahitaji mfumo wa tahadhari ya mapema ili mamlaka ziweze kuona wakati wa taratibu za uombaji wa hifadhi ambapo kuna matatizo’.
Bi. Merkel alimalizia kwa kusema: ‘Tutachukua hatua zote stahiki na kuhakikisha hali ya usalama kwa wananchi wetu. Tutaichukulia kwa umakini mkubwa sana changamoto ya muingiliano’.

LEAVE A REPLY