Meneja wa hoteli afunguka Ebitoke kuvamia mkutano wa Mlela

0
474

Baada ya Muigizaji wa vichekesho nchini, Ebitoke kusababisha vurugu kwenye mkutano wa Muigizaji Yusuph Mlela na waandishi wa habari uliofanyika leo Novemba 11 katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam kuna habari nyingine zimeibuka.

Meneja wa hoteli hiyo, aliyejitambulisha kwa jina Suleiman Victor, ambaye alieleza kuwa kulikuwepo na mpango uliohisiwa kuhusishwa na tukio hilo lililosababisha hasara na uharibifu wa vitu kadhaa kutokana na fujo hizo.

Meneja Suleiman alieleza kuwa Novemba 10, Mlela afika katika ofisi za hoteli hilo na kufanya ‘Booking’ kwa ajili ya mkutano huo na katika mazungumzo ya hapa na pale alinukuliwa katika maelezo kuwa kuna mchezo wataufanya.

Hata hivyo mpaka sasa haijabainika kama mpango huo ulilenga kufanyika kwa tukio hilo la vurungu ingawa katika maelezo ya juu juu, Yusuph Mlela alidai kuwa hakutegemea kama Ebitoke angefanya vurugu hizo.

Ikumbukwe wawili hao kati ya Ebitoke na Mlela hivi karibuni walikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na kuonekana sehemu mbalimbali wakiwa pamoja.

LEAVE A REPLY