Meneja wa Diamond, Salam SK akutwa na virusi vya Corona

0
180

Meneja wa msanii Diamond Platnumz Salam SK amethibitisha kupata virusi vya Corona na yupo chini ya Uangalizi Maalum Kuanzia Juzi kwa ajili ya uchunguzi.

Kupitia Ukurasa wake ww Instagram, Ameeleza Kuwa – Napenda kuwajulisha na kuwatoa hofu ndugu, jamaa na marafiki kuwa nimepata majibu ya vipimo na nimeonekana nikiwa na Corona Virus, kwa sasa nipo chini ya uwangalizi mzuri na afya yangu inaendelea vizuri.

Salam SK ameongeza pia – niishukuru serikali kwa maandalizi mazuri na huduma nayopata wodini, Kwenye kituo toka juzi nipo peke yangu kama nimekikodisha vile.

Pia ameendelea kusema kuwa wahudumu wanaushirikiano mzuri Mungu awalinde na awape afya njema maana wamejitolea nafasi zao kutupatia huduma sisi waathirika.

Hili janga la kimataifa linakwepeka kama tutafuata ushauri nasaha kutoka kwenye Wizara husika, naomba kwa wote tuwe salama na familia zetu, tuchukue tahadhari mapema.

LEAVE A REPLY