Meneja Max Rioba atamani kufanya kazi na Alikiba

0
23

Meneja wa wasanii nchini, Max Rioba amefunguka na kusema kuwa anatamani kufanya kazi na msanii wa Bongo Fleva, Alikiba kwani ni mtu mwenye kipaji kikubwa.

Max Rioba ambaye kwasasa ni meneja wa Hamisa Mobeto amesema kuwa ana imani kama atakuwa meneja wa Alikiba basi watatengeneza pesa, kufanya makubwa na kuboresha muziki.

Sababu za kutamani kufanya kazi na Alikiba ni aina ya uimbaji wake ambapo anaamini itakuwa nzuri kibiashara kwa upande wao kama watafikia makubaliano.

Amesema kuwa anatamani sana kufanya naye kazi kwa sababu jamaa ni muimbaji sana na anaweza, njia zake anazoenda yeye anaona kama zinafaa lakini naamini kuna haja ya ladha fulani hivi ambapo kwake hakipo”.

Pia Max Rioba amesema muziki wa sasa unaboa kwani wote wanaimba style moja ndiyo maana haudumu kutokana na kutokuwa bora.

LEAVE A REPLY