Meneja ‘atafuna kifedhuli’ 16bn za wasanii wake

0
129

Meneja wa zamani wa biashara wa staa wa Pop Alanis Morissette amekiri kuiba zaidi ya $7m (TZS16bn) kutoka kwa staa huyo na mastaa wengine.

Meneja huyo, Jonathan Schwartz anayekabiliwa na mashtaka ya ubadhirifu baada ya kugunduilika kwa mchezo mchafu aliokuwa anaufanya wa kuhamishia pesa za msanii huyo kwenye akaunti yake binafsi.

Staa huyo mzaliwa wa Canada alipomkabili meneja huyo kwa mara ya kwanza alidanganya kuwa ametumia pesa hizo kwenye uwekezaji wa biashara haramu ya bhangi ambayo ilikuwa inashamiri.

Meneja huyo ambaye alikuwa na jukumu la kukusanya mapato ya msanii huyo, kusimamia akaunti za fedha za staa huyo pamoja na kuandaa malipo kwa niaba ya msanii huyo alikabidhisha nyaraka za usimamizi aliokuwa anaufanya kati ya mwaka 2009 na 2016.

Wakili wa meneja huyo Nathan Hochman amekiri kuwa mteja wake amekubali kufanya makosa hayo kwa kuchukua $4.8m (TZS 9bn) kutoka kwenye akaunti ya Morissette na zaidi ya $2m (TZS 4bn) kutoka kwa mastaa wengine ambao hata hivyo hawakuwekwa wazi.

Ngoma za Morissette zilizompa umaaruf mkubwa ni pamoja na ‘Ironic na You Oughta Know’.

LEAVE A REPLY