Meja Kunta amponza mama yake

0
171

Msanii wa Singeli Meja Kunta amefunguka na kusema kashfa na kiki zilizotokea zimemsababishia mama yake mzazi kutokuwa sawa kiafya.

Meja Kunta amesema , “Kwa upande wangu hata mimi sizipendi, kitu ambacho ningeweza kufanya labda ni kuitisha watu au vyombo vya habari na nikaliongelea lile suala ili kujitoa na jinsi gani ya kujisafisha ili nisionekane mbaya”.

“Kilichofanyika kimemuumiza sana Meja na kimemsababishia matatizo hadi kwa Mama yangu mzazi kwa sababu, hadi leo hii hayupo sawa amekuwa ni mtu wa kuanguka kiufupi hayupo sawa.

Amesema kitu ambacho kinanipa  mawazo sana kwa sababu sikuwahi kufirikia hata siku moja kama naweza kusababisha matatizo”.

LEAVE A REPLY