Meek Mill na Nicki Minaj warushiana maneno mtandaoni

0
80

Vita ya maneno kati ya Meek Mill na Nicki Minaj imerudi tena, usiku wa kuamkia leo ulikuwa wa moto sana huko twitter.

Vita hiyo ya maneno ilianza baada ya LIKE ya Meek Mill kukutwa kwenye moja ya ‘Meme’ ya mume wa Nicki Minaj, Kenny Petty ambayo iliwekwa hapa instagram na akaunti moja ya shabiki wa Nicki Minaj.

Hii ilimfikia Minaj ambaye aliibuka na kuanza kumjibu Meek Mill akimwambia ni kitu gani kinamfanya asiendelee na maisha yake anabaki kumfatilia hadi leo.

Pia alimrushia maneno kuwa ananyanyasa wanawake kwa kuwapiga, akitoa ushahidi kwamba Meek Mill aliwahi kumpiga Dada yake huku akijirekodi.

Tuhuma za kupiga wanawake hazikuwa nzuri kwa Meek Mill ambaye aliibuka na mfululizo wa tweets kibao akijitetea na kumchana Ex wake huyo kuwa ni mpuuzi na mnyanyasaji kwa wanawake wenzake.

Pia Meek alisema kuwa Nicki Minaj aliwahonga Wanasheria ili waifute kesi ya Kaka yake (Jerani Maraj) ambaye wiki iliyopita alihukumiwa kifungo cha maisha Jela kwa Ubakaji.

LEAVE A REPLY