Meek Mill ashtakiwa kwa kuiba mashairi

0
74

Mwanamuziki wa Marekani, Meek Mill ameshtakiwa na kampuni ya Dream Rich Entertainment kwa kuiba mashairi na kuyatumia kwenye nyimbo zake mbili.

Dream Rich ambayo ni label ya muziki toka Philadelphia, imemfungulia mashtaka hayo Meek Mill, Dream Chasers pamoja na Atlantic Records kwa ukiukaji wa hakimiliki akidaiwa kuiba mashairi kutoka kwa mtunzi ambaye aliunganishwa naye kupitia label hiyo.

Meek Mill anadaiwa alipata nafasi ya kuingia kwenye mafaili ya mtunzi huyo na kujipakulia mashairi ambayo aliyatumia kwenye ngoma zake; 100 Summers na Cold Hearted II ambazo zipo kwenye album yake ‘Championships’ bila ridhaa ya wahusika.

Dream Rich wanadai fidia ya kiasi cha ($300,000) sawa na TSH. Milioni 695 kutokana kwa mwanamuziki huyo ambaye anadaiwa fidia hiyo.

 

LEAVE A REPLY