Mediocre ya Alikiba yaingia 10 bora ya Afrika

0
43

Wimbo mpya ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, AliKiba iitwayo ‘Mediocre’ imetajwa kwenye orodha ya nyimbo 10 bora Afrika kwa mwezi Septemba zinazofanya vizuri.

Wimbo huo ambao ulitoka Alhamisi iliyopita imewekwa kwenye nafasi ya 6 na kumfanya AliKiba kuwa msanii pekee wa Tanzania na Afrika Mashariki kutokea kwenye orodha hiyo.

Orodha hiyo imetolewa na ukurasa wa twitter uitwao African Music Promotion, ikizitaja ngoma za wakali kama Wizkid, Cassper Nyovest, Sarkodie na Davido ambaye ali-retweet baada ya ‘Fem’ kutajwa namba 1.

Wimbo huo umepokelewa vizuri na mashabiki wa msanii huyo kutokana na alichokiimba ndani ya wimbo huo mpya wa mkali huyo wa Bongo Fleva.

LEAVE A REPLY